Wachezaji wa Tanzania na Kenya wakiwa katika mashindano ya wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki leo, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume
jijini Arusha, mechi hiyo ilivuta hisia za wakazi wa jiji hilo
waliomiminika kuja kushuhudia wabunge hao wakimenyana uwanjani, baada ya
dakika ya tano bunge la kenya walijipatia
bao la kwanza, bao lililofungwa na Mh.Steven Nyatta na hatimaye
Tanzania kusawazisha dakika ya 24 kwa njia ya penalt baada ya Mh.Mbunge
Joshua Nassari kudondoshwa eneo la hatari kwa kugongwa na mlinda mlango
wa kenya Kega Kanin.
Mlinda mlango wa Timu ya kenya Kega Kanin akijaribu kuzuia goli lililopatikana kwa njia ya penalt katika dakika ya 24 .
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akichechemea uwanjani baada ya kuanguka na kupewa huduma ya kwanza.
Wachezaji wa timu ya Tanzania wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza
Wachezaji wa timu ya Kenya wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza.
No comments:
Post a Comment