Naibu waziri wa fedha Adam Malima akimkabidhi meneja wa fedha
wa benki ya CRDB Sosteness Biseko
tuzo ya NBAA ya ushindi katika
uandaaji wa taarifa bora za fedha mwaka 2013-2014,jumla ya benki tisa
zilishiriki ambapo Benki ya CRDB iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la
mabenki, hafla hiyo ilifanyika juzi katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha
*********
Mashirika binafsi ,taasisi
na idara mbalimbali za serikali zimehimizwa kushiriki katika mashindano ya tuzo
zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA katika
uandaaji bora wa taarifa za fedha za mwaka ili kuboresha hesabu za mashiriki
hayo na kuongeza uwazi katika shughuli za biashara za ndani ya nchi na
kimataifa
Mwenyekiti
wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA Profesa Issaya Jairo ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati wa kufunga mkutano mkuu wa mwaka wa bodi hiyo ulio enda
sambamba na utoaji wa tuzo na vyeti kwa washindi katika uaandaaji bora wa taarifa za fedha za mwaka ambapo kwa
mwaka 2014 jumla ya washiriki 40 walishiriki ambao waligawanywa katika makundi
11 kulingana na huduma wanayo itoa
Katika kundi
la mabenki, benki ya crdb ilibuka mshindi wa kwanza kwa mwaka2013-2014 na kupata tuzo
maalumu ya uandaaji wa taarifa bora za fedha za mwaka iliyokabidhiwa na naibu
waziri wa fehda Adam Malima kwa meneja
wa fedha wa benki hiyo Sosthenes Biseko ambaye akizungumzia ushindi huo amesema
ni njia mojawapo ya kuudhihirishia umma wa watanzania kuendelea kuwa na Imani na
benki.
Wafanyakazi mbalimbali wa benki ya CRDB wakiwa katika picha wakati wa makabidhiano hayo.
No comments:
Post a Comment