Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 8, 2014

DIAMOND TENAAAA...ASHINDA TUZO YA FUTURE AWARDS HUKO NIGERIA

Tuzo ya Msanii DIamond Platnumz aliyoshinda Nchini Nigeria 

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Abdul Nassib almaarufu kama Diamond Platnumz Anyakua tuzo nyingine ya The Future Awards zilizokuwa zikifanyika leo usiku huko Lagos Nigeria kwa Kina Msanii Davido

Ikiwa usiku huo huo ambao Mshiriki wa Tanzania katika Big Brother Africa Idris Sultan anatangazwa Mshindi Na Huko Lagos Nigeria Diamond Platnumz naye akatangazwa mshindi wa Tuzo hizo za Te Future Award 2014.

Mara baada ya Mshiriki wa Tanzania Katika Shindano la Big Brother Africa 2014 Idris Sultan kutangazwa MShindi watanzania wengi walionekana kufurahishwa sana na Ushindi wake huku wengine Wakimpongeza kupitia ukurasa wao wa Tweeter muda mfupi baadae Msanii Kutoka Nchini Nigeria Davido alionekana waziwazi kukerwa na Ushindi huu wa Mtanzania Idris na kuamua kutweet "N They Cheat Again lol". Tweet hii imemfanya Msanii huyo wa NIgeria kushambuliwa na Maneno na watanzania wengi katika kurasa zao za tweeter.


Mara baada ya Kutweet "N They Cheat Again Lol" tweet hiyo imesomeka pia Mara baada ya Kuibuka tena Mshindi katika Tuzo Hizo za The Future Awards 2014 zilizokuwa zikifanyika Jijini Lagos Nchini Nigeria ambapo ni nyumbani kwa Msanii Davido.

Usiku wa leo Utakumbukwa sana na Watanzania kutokana na Kuwa Usiku mzuri kwa Watanzania na Tanzania Kwa Ujumla kwa maana ni usiku ambao Mshiriki kutoka Tanzania ambae alikuwa akishiriki Shindano la Big Brother Africa Idris Sultan kutangazwa Mshindi wa Shindano hilo kwa Mwaka 2014 na kuondoka na kitita cha Dola za Kimarekani laki tatu usiku huo huo na Diamond Platnumz kutangazwa Mshindi wa Tuzo ya The Future awards 2014

Hongereni watanzani kwa kutufanya kumaliza Mwaka 2014 vizuri huku Davido akionyesha chuki zake binafsi dhidi ya watanzania na Tanzania Kwa Ujumla

No comments:

Post a Comment