Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 29, 2014

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS KUPELEKA MATAMASHA MENGINE MJINI SONGEA, NI KUTOKANA NA MWITIKIO WA WANASONGEA‏

1
Mwimbaji wa Muziki wa injili Upendo Nkone akiimba mbele ya mashabiki wa muziki huo kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo tamasha kubwa la Krismas limefanyika na kushirikisha waimbaji mbalimbali kutoka nchini na nje ya Tanzania, onesha la leo lilikuwa ni hitimisho la matamasha ya Krismas yaliyofanyika katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma yakishirikisha waimbaji kama Upendo Nkone, Faraja Ntaboba kutoka nchini DRC Congo , Edson Mwasabwite.
Wngine ni Ambwene Mwasongwe, Bonny Mwaiteje, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa Kutoka nchini DRC Congo , Tumaini Njole, Titha Mutinda kutoka nchini Kenya Joshua Mlelwa na wengine wengi.Tamasha la leo lilikuwa ni la kwanza kufanyika mjini Songea na Mwandaaji wa tamasha hilo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama, amesema kampuni hiyo inatarajia kufanya matamasha mengine ya injili katika mkoa huo wakati ujao kutokana na mwitikio wa watu wa Songea.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SONGEA) 2
Mwimbaji Upendo Kirahilo akipagawisha mashabiki wake wakati alipokuwa akiimba jukwaani katika tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo. 3
Mwimbaji Upendo Kirahilo akipagawisha mashabiki wake wakati alipokuwa akiimba jukwaani katika tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo. 6
Mwimbaji Upendo Kirahilo akserebeka na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama alipokuwa akiimba jukwaani katika tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo. 



8Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na MC wa Tamasha hilo Bw. Mwakipesile wakielekea kumtunza mwimbaji wa muziki wa injili Joshua Mlelwa wakati alipokuwa akionyesha uwezo wake jukwaani kwenye tamasha la Krismas lililofanyika mjini Songea leo. 11
Mgeni rasmi wa tamasha hilo Meya wa mji wa Songea Mh. Charles Mhagama akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili kwenye uwanja wa majimaji kutoka kushoto ni Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo John Melele. MC Mwakipesile na Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion. 9
Mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje nakipagawisha mashabiki wake kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea leo. 10
Mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje nakipagawisha mashabiki wake kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea leo. 12
Somlomon Mkukubwa akiimba wimbo unaoelezea kisa cha mkono wake kukatwa ambao unamuelezea mama wa kambo aliyesababisha tukio hilo na kuwaasa mashabiki wake kusamehe kama yeye alivyomsamehe mama yake wa kambo 13
Mashabiki wakiimba pamoja na mwimbajo Solomon Mukubwa 01
Mwimbaji Ambwene Mwasongwe akiimba kwa hisia huku akishirikiana na mwimbaji Solomon Mukubwa wakati wa tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo kutoka kushoto ni Edson Mwasabwite na Faraja Ntaboba kutoka nchini DRC Congo.

No comments:

Post a Comment