Taarifa ya mahakama ya ICC, kutupilia mbali kesi dhidi ya
Uhuru Kenyatta, imepokelwa na watu wengi nchini Kenya kwa hisia mseto.
Baadhi wanahisi kuwa waathiriwa wa ghasia za baada ya
uchaguzi watakosa haki ingawa baadhi wanahisi kwua Uhuru Kenyatta hakupaswa
hata kufikishwa ICC tangu hapo.
Lakini swali ni jee Rais Kenyatta alipokea vipi habari hiyo?
Rais Uhuru Kenyatta
Haya ndio aliyokuwa nayo ya kusema kwenye akaunto yake ya
Twitter:
''Nimepokea habari kwamba kiongozi wa mashitaka ICC
ametupilia mbali kesi dhidi yangu ........''
''Daima nimekuwa nikisema kuwa kesi za Kenya ICC
ziliharakishwa sana kupelkewa katika mahakama ya ICC bila kufanyiwa uchunguzi
wa kina.
"moyo wangu hauna shauku hata kjidogo. ''
"mara kwa mara nimekuwa nikiwasisitizia wakenya na
dunia nzima kuwa sina hatua. ''
"uamuzi huu ni afueni kubwa sana kwangu kwani ulipaswa
kutolewa miaka sita iliyopita. Umechelewa sana ''
''Nimefurahishwa sana na habari hizi ambazo nimekuwa
nikizisubiri tangu jina langu kuhusishwa na kesi iliyowasilishwa Hague dhidi
yangu.''
''Kadhalika Naibu wangu William Ruto ni kiungo muhimu sana
kwa serikali yangu na ninathamini umuhimu wake''
No comments:
Post a Comment