Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, December 7, 2014

KIBADENI AZUSHIWA KIFO, YEYE AWAOMBA RADHI WALIOPATA USUMBUFU

Kocha maarufu nchini, Abdallah ‘King’ Kibadeni amezushiwa kifo na kusababisha utata mkubwa.
Taarifa ziliripotiwa na mtandao mmoja zimefanya watu waanze kumpigia simu kila mara.
“Kweli hata mimi napigiwa simu na watu wengi sana kama nimefariki dunia, hawa watu sijui wamepata wapi hizi taarifa.
“Kweli siku chache zilizopita nimefanyiwa upasuaji wa jicho. Hadi sasa niko safi kabisa, ninaendesha hata gari.

“Kupitia mtandao wako, naomba niseme hivi; ninawaomba radhi wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizi,” alisema Kibadeni na kuongeza.





“Ila ninaomba wale ambao wanaopata taarifa ni vizuri kuzihakikisha kuliko kusababisha usumbufu kwa watu.SALEHE JEMBE BLOG

No comments:

Post a Comment