Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 16, 2014

MAKOMANDO WAWAOKOA MATEKA SYDNEY, WAMUUA MTEKAJI

Huyu ndiye mtekaji raia wa Iran, Haron Monis.
WATU watatu wameuawa akiwemo mtekaji raia wa Iran, Haron Monis aliyekuwa ameteka watu kwa zaidi ya saa 16 katika mgahawa mmoja jijini Sydney nchini Australia jana baada ya Makomando kuvamia eneo hilo. Watu wanne akiwemo polisi wamejeruhiwa wakati wa zoezi la uokoaji.
Mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza.
Mtekaji huyo alikuwa ameachiwa kwa dhamana kwa makosa mbalimbali aliyokuwa ameshitakiwa nayo. Moja ya makosa yake ilikuwa kuwatumia barua ya matusi wazazi wa wanajeshi wa Australia 



waliofariki wakiwa wanalitumikia jeshi la taifa hilo nchini Iraq.
Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott alisema lilikuwa jambo la kushtua sana kwamba wananchi wasio na hatia kutekwa nyara na mtu ambaye alikuwa anashinikizwa kisiasa.
Makomando walifyatua risasi na kisha kuingia ndani ya mgahawa huo huku wakirusha magurunedi.

No comments:

Post a Comment