Mgonjwa
Hashimu Mohammed Mollel (28) anayetuhumiwa kumuua mgonjwa mwenzake,
Lazaro Mollel (75) aliyelazwa naye katika Hospitali ya Mkoa ya Mount
Meru,Arusha.
Joseph Ngilisho, Arusha MAAJABU! Katika hali isiyo ya kawaida mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, akisumbuliwa na maradhi ya mguu, Hashimu Mohammed Mollel (28), (pichani) mkazi wa Lemala, Arusha amemuua mgonjwa mwenzake aliyelazwa naye, Lazaro Mollel (75) kwa kumpiga na chuma cha kutundikia dripu.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Novemba 22, mwaka huu saa 6 usiku katika wodi ya majeruhi baada ya mtuhumiwa huyo kuzua tafrani kwa kutaka kupiga wenzake, hali iliyosababisha wagonjwa mbalimbali kutimua mbio na kujificha kuokoa maisha yao na kumuacha marehemu ambaye alikuwa hajiwezi akiwa amelala kitandani.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Novemba 22, mwaka huu saa 6 usiku katika wodi ya majeruhi baada ya mtuhumiwa huyo kuzua tafrani kwa kutaka kupiga wenzake, hali iliyosababisha wagonjwa mbalimbali kutimua mbio na kujificha kuokoa maisha yao na kumuacha marehemu ambaye alikuwa hajiwezi akiwa amelala kitandani.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa, Hashimu ambaye
bado amelazwa katika wodi hiyo akiwa amefungwa pingu mkononi, chini ya
ulinzi wa polisi, alieleza kuwa mnamo muda huo mtuhumiwa alitenda kosa
hilo baada ya kumaliza kuswali.
‘’Kabla ya kuanza swala mtuhumiwa huyo alimuomba kijana aliyekuwa
akimuuguza ampeleke kujisaidia,” alisema shuhuda huyo ambaye hakutaka
jina lake kuandikwa gazetini.
Aliongeza kuwa baada ya kurejea alipiga magoti na kuanza kuswali
chini ya kitanda alichokuwa amelazwa na baadaye alipomaliza aliwaamuru
wagonjwa wenzake wazime taa.
“Baada ya taa hizo za wodini kuzimwa mtuhumiwa alisikika
“Baada ya taa hizo za wodini kuzimwa mtuhumiwa alisikika
akisema kwa sauti kubwa kuwa leo anataka kuua mtu huku
akivurugavuruga vitu kwenye vitanda vya wagonjwa kikiwemo cha kwake na
kupiga kelele kwa sauti kubwa, hali iliyowafanya wagonjwa wengine
kutimua mbio. Hata hivyo, wakati vurugu hizo zikiendelea muuguzi wa zamu
alitoa taarifa kwa kupiga simu kituo cha polisi mjini kati.
Wakati askari polisi wakisubiriwa mtuhumiwa aliendelea na vurugu na
kuchukua chuma cha kutundikia drip na kuivunja kisha kwenda kumpiga
kichwani marehemu aliyekuwa amelala pekee kwenye wodi hiyo akiuguza mguu
wake wa kulia na alifariki dunia papo hapo.
Polisi walipofika walikuta ameshaua na alikamatwa na kuchomwa sindano
ya dawa ya usingizi, ndipo akadhibitiwa.Mganga mkuu wa hospitali hiyo,
Josian Mlay alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa
mtuhumiwa huyo hakuwa na matatizo yoyote ya akili. Kamanda wa Polisi
mkoani Arusha, SACP Liberatus Sabas alikiri kutokea kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment