Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 15, 2014

MTU MWENYE SILAHA AENDELEA KUSHIKILIA MATEKA KWENYE MGAHAWA MJINI SYDNEY,NCHINI AUSTRALIA


Polisi wakimpokea msichana aliyekuwa ndani ya mgahawa huo
Mtekaji huyo anadaiwa kuwasiliana na vyombo vya habari kupitia mateka hao akitaka apewe bendera ya ISIS na pia simu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott.
Watu watano wamekimbia kutoka kwenye mgahawa huo uliopo katikati ya mji wa Sydney, Australia ambako mtu mmoja mwenye silaha anashikilia mateka. Bado watu watu wasiojulikana idadi yake wanaendelea kushikiliwa kwenye mgahawa huo.
Mamia ya polisi wameuzingira mgahawa huo na kufunga mtaa huo wenye watu wengi.
Picha mbalimbali zimeonekana zinazoaminika kuwa mateka walioweka mikono yao juu ya vioo vya mgahawa huo wa Lindt Chocolate. Video zimewaonesha mateka hao wakiwa wameshika bendera nyeusi yenye maneno ya kiarabu yanayosomeka:


“There is no God but God and Mohammed is the prophet of God.” Bado haijulikani sababu za utekaji huo.
“Hatujui kama tukio hilo ni la kisiasa, ingawa ni wazi kuna dalili linaweza kuwa,” waziri mkuu wa Australia, Tony Abbott aliwaeleza waandishi wa habari.
Maneno hayo ya kiislamu kwenye bendera hiyo yamezusha hofu kubwa kuwa tukio hilo mjini Sydney linaweza kuhusishwa na waislam wenye msimamo mkali.

No comments:

Post a Comment