Feisal Mohamed Ally
Polisi wa kimataifa , interpol tawi la Tanzania wamemkamata
mfanya biashara maarufu raia wa Kenya kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili na
uhalifu uliovuka mipaka ,hususan mauaji ya tembo .
mtuhumiwa huyo Mohamed Ally Feisal Amekamatwa mjini
Dar-Es-Salaam baada ya kusakwa kwa kipindi kirefu kwa makosa hayo ya kimataifa
kutoka Dar Regina Mziwanda anaarifu zaidi.
Akitbibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Bwana Diwani
Athumani kutoka kamisheni ya Kurugenzi ya makos aya jinai amesema mtuhumiwa
huyo anakabiliwa na tuhuma za kujihusisha na
vitendo vya uhalifu wa kimataifa
ikiwemo uwindaji wa uliovuka mipaka kimataifa katika nchi mbali mbali)
Bwana Athumani Diwani alieleza kuwa kwa sasa mtuhumiwa huyo
anashikiliwa huku upelelezi ukiendelea kujua makosa mengine aliyoyafanya
kuhusiana na biashara za bidhaa zitokanazo na Tembo ndani ya Tanzania na katika
nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo nchi yake ya asili Kenya.
Mohamed Feisal Ally amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa
tuhuma za uwindaji haramu husani mauaji ya Tembo tatizo ambalo ni kubwa
hususani katika ukanda huu wa Afrika Mashariki hasa Kenya na Tanzania ambapo
idadi kubwa ya Tembo wamekuwa wakiuawa kila mwaka na kutishia kutoweka kwa
viumbe hao.
No comments:
Post a Comment