Mtandao wa facebook.Mwanablogu wa kenya Robert Alai
ameshtakiwa nchini Kenya kwa kutumia mtandao wa kijamii twitter Kumtusi rais.
Mwanablogu maarufu lakini anayezusha mzozo Kenya ameshtakiwa
kwa kumdharau rais, kufuatia ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii
twitter mapema wiki hii.
Robert Alai anashutumiwa kwa kumuita Uhuru Kenyatta rais
ambaye haja komaa kupitia ukurasa wake wa twitter.
Amekana mashtaka na akaachiliwa kwa dhamana ya dola elfu
mbili.
Robert Alai amekumbwa na mzozo mara kadhaa kutokana na
anayoyaandika kwenye ukurasa wake
wa twitter.
Miaka miwili iliyopita alikamatwa na kuhojiwa kwa kutuhumu
kwamba msemaji wa serikali anapanga kumuua.
Leo amefikishwa mahakamani kukabiliwa na mashtaka ya kunuia
kumtusi rais.
Waendesha mashtaka wameiambia mahakama kwamba huenda
wakaongeza mashtaka dhidi yake punde uchunguzi utakapokamilika.
Wakili wake ambaye ni seneta maarufu Kenya, amepinga jaribio
la serikali kumnyima dhamana.
Hakimu anayesikiliza kesi amemuamuru kutoandika ujumbe kama
huo katika mitandao yote ya kijamii wakati uchunguzi na kesi dhidi yake
inpoendelea.
Alai ana wafuasi zaidi ya laki moja kwenye ukurasa wake wa
twitter, na anatambulika kwa kuwa mkosoaji mkali wa serikali.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment