Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 17, 2014

Mwingerea hatiani kwa kuwalawiti watoto Kenya

Mwalimu wa shule ya umma nchini Uingereza amepatikana na hatia ya kuwalawiti watoto wanaorandaranda mitaani nchini Kenya.
Simon Harris alipatikana na hatia ya makosa saba, ikiwemo kuwadhulumu kingono watoto hao katika mji wa Gilgil.
Alipatikana na hatia katika mahakama ya Birmingham kwa makosa manne ya kumiliki picha chafu zinazoonyesha uchi wa waoto wadogo.
Hata hivyo mahakama haikumpata na hatia ya kitendo cha kuwabaka watoto hao.
Haris alikuwa anakabiliwa na maskosa 23 ikiwemo madai 18 ya kuwadhulumu watoto.


Unyama huo ulitendwa wakati Harris alipokuwa anaendesha shirika la kijamii la kuwasaidia watu mapema mwaka wa 1990.
Wakati kesi yake ilipokua inaendelea, wendesha mashitaka walisema kuwa aliwahadaa watoto hao wavulana kwenda nye nyumbani kwake iliyojulikana kama "The Green House", kwa kuwapa chakula na kuwapa hifadhi.
Kabla ya kesi hio kuanza, Harris alikiri makosa sita ya kuwadhuru watoto hao waliokuwa kati ya umri wa miaka 13-14 alipokuwa bado mwalimu wa chuo cha Davon.

Awali alikuwa anakabiliwa na makosa 22 kuhusiana na dhuluma hizo alizozitenda nchini Kenya lakini jaji Philip Parker QC alisema kuwa makosa manne dhidi ya mtuhumiwa yaliodnolewa wakati kesi hio ilipokuwa inasikilizwa.chanzo bbc

No comments:

Post a Comment