Mjeshi huyo akiwa amepata fahamu baada ya kumwagiwa maji
Mjeshi akiwa amezima kwa kunywa pombe kupita kiasi
KATIKA hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga
Taifa (JKT) anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa usiku wa juzi amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada ya
kukutwa amelewa chakali na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo la nje ya
stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa
Tukio hilo lilitokea muda wa saa 2 usiku baada ya wasamaria
wema kumshusha askari huyo kutoka katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda
kutoka Mafinga kuja mjini Iringa.
Akisimulia kisa na mkasa wa askari huyo kulewa chakali kiasi
cha kushindwa kujitambua mmoja kati ya wasamaria wema aliyejitolea kumshusha
katika basi hilo alisema kuwa askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa
amelewa na wakati wote wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha
kushindwa kujimudu na kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi
hilo.
Hata hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu
kujitambua hivyo kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa
maji kabla ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji machafu
.
Alisema kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa
namba ya ndugu yake ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru
kuvuliwa nguo na kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana akilishushia
heshima jeshi kwa ulevi uliopitiliza
" Umelidhalilisha sana jeshi kwa askari kulewa hivi
ukiwa katika sare .....sasa nataka kukuvua sare kisha nakupeleka kulala polisi
kabla ya kesho kukuchukulia hatua zaidi " alisikika akisema kiongozi huyo
ambae jina wala cheo chake hakukitaja
Maamuzi hayo ya kiongozi wake yaliwafanya mashuhuda
kumuangukia na kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo sana mambi ambayo
aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na kumpeleka eneo la Kihesa .
Ushauri wetu kwa askari wetu kujaribu kuheshimu nafasi hizo
japo hakuna anayewakataza kunywa pombe ila watambue kuwa unywaji pombe kupita
kiasi ni hatari kwa afya yako ama chonde chonde ulevi noma.
No comments:
Post a Comment