Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, December 13, 2014

PICHA::AKUTWA AMEJINYONGA PORINI MKOANI TANGA



Sehemu ya Wananchi wakazi wa Mji wa Pongwe Mkoani Tanga wakiangalia mwili wa mtu huyo uliokuwa ukining'inia juu ya mti.Ambapo mpaka ripota wetu anaondoka eneo la tukio hakukuwa na Mwanausalama yeyote aliefika eneo hilo.
Wakazi wa Mji wa Pongwe wakiuangalia mji huo kwa masikitiko makubwa.





Ni uzuni ulikuwa imetawala eneo hilo.
Kila aliepata taarifa hiyo alienda kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo.

MTU mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 27 mpaka 30 ambaye jina lake halijafahamika mpaka sasa amekutwa akining'inia juu ya mti wa Mwembe uliopo katika pori lililopo nje kidogo ya mji wa Pongwe,Mkoani Tanga akidhaniwa kuwa amejinyonga.

Hali ya sintofahamu iliendelea kutanda katika eneo hilo huku kila alieweza kufika katika eneo hilo la tukio akiwa na mshangao wa kipi kilichomsibu mtu huyo mpaka kufikwa na mauti ya aina hiyo.

Akizungumza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaja jina lake,ameeleza kuwa walipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa kijana mmoja aliekuwa akichunga ng'ombe katika pori hilo ambaye jina lake halikuweza fahamika mara moja,hali iliyowapekea kwenda moja kwa moja eneo la tukio kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo,lakini kila alefika pale hakuweza kumtambua huku wengine wakisema huenda hutu huyo alikuwa ni mgeni kijijini hapo.

Ripota wetu alipo Jijini Tanga anaendele na juhudi za kumtafuta Kamana wa Polisi wa Mkoa huo ili kuona kama anataarifa zozote juu ya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment