Ripoti ya kamati ya bunge la Seneti nchini Marekani imekosoa
vikali mbinu zinazotumiwa na Shirika la Ujasusi la nchi hiyo za kuwahoji
washukiwa wa uhalifu na kuelezea kwamba ni za kikatili na zisizofaa.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama ya bunge la seneti Dianne
Feinstein amesema katika baadhi ya matukio wanavyotendewa washukiwa hao ni sawa
na mateso.
''Watu waliowekwa kizuizini walipaswa kutii mbinu zilizokuwa
zikitumiwa, kuvuliwa nguo na kuachwa watupu, walikuwa wakiwekwa katika hali ya
mateso ya muda mrefu.
Shirika la Ujasusi la marekani, CIA tuhumani
Walikuwa wakizuiwa kulala kwa siku kadhaa, hadi saa 180-
ikiwa ni sawa na siku saba na nusu, zaidi ya wiki bila ya kulala, kawaida
wakiwa wamwesimama au katika hali ya kuwachosha na wakati huohuo mikono yao
ikiwa imefungwa pamoja juuya vichwa.
Mbonu hizo za utesaji zilianzishwa baada ya shambulio la
kigaidi la Septemba 11, mwaka 2001 nchini Marekani...''
Mbinu hizo zinazotumiwa na shirika hilo la ujasusi
zimeelezwa na wabunge hao wa seneti kuwa zinamapungufu na kwamba CIA imekuwa
ikitoa taarifa zisizo sahihi kwa umma.
No comments:
Post a Comment