Watu 2 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa na wananchi
wenye hasira mkoani Tanga.
Wakielezea vyema tukio hilo baadhi ya wafanyakazi na walinzi
wa kiwanda hicho wamesema majambazi hao baada ya kuingia ndani ya geti la
kiwanda hicho walikwenda moja kwa moja katika chumba cha mhasibu na walipofika
walianza kunyonga mhasibu lakini wakati wa kujitetea ndipo sekretari wa mhasibu
alipotoka nje ya ofii na kupiga mayoe kuashiria bosi wake amevamiwa na
majambazi.
Kufuatia hatua hiyo mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda
hicho Bwana Amiry Ramadhani ameliomba jeshi la polisi mkoani Tanga kuhakikisha
wanafanya upepelezi wa kutosha ili kujua kama huenda kuna baadhi ya wafanyakazi
ambao wamekuwa chanzo cha tukio hilo.
No comments:
Post a Comment