Sigara ya kielektroniki iliyo na bangi ndani yake imeanza
kuuzwa nchini Uingereza.
Wakati sigara ya kwanza ya bangi ya kieletcroniki
ilipozinduliwa mnamo mwezi juni ilikuwa ikipatikana ughaibuni pekee.
lakini sasa ,kampuni moja imechukua hatua zaidi na kuanza
kuuza bidhaa hiyo katika maeneo ya Uingereza.
KanaVape kama kinavyojulikana ni kifaa ambacho kina fanana
na sigara za kielektroniki lakini chenye Bangi, kitauzwa mitandaoni kuanzia
alhamisi ijayo,kulingana na mtandao wa Metro nchini Uingereza.
Watengezaji wa bidhaa hiyo nchini Uingereza Atonin
Cohen na
Sebastien Beguerie wanadai kwamba bidhaa hiyo ni halali kwa kuwa haina kemikali
za bangi zinazoathiri akili.
Bidhaa hiyo inatumia asilimia tano ya bangi,ikimaanisha kuwa
inampa mteja hisia za utulivu kama bangi lakini haina athari zozote mbaya.
Bidhaa hiyo ya E-joint inamaanisha kuwa mtumiaji anaweza
kuvuta mvuke wa bangi bila kupata harufu ya kawaida ya moshi wake.
Mashirika ya madawa hatahivyo yameipinga bidhaa hiyo kama
kitu kilichotengezwa ili kuvutia hisia,lakini yakasema kuwa kuna uwezekano
mkubwa kwamba bidhaa hiyo itakuwa halali chini ya sheria ya Uingereza kwa kuwa
haina kemikali yenye madhara.
No comments:
Post a Comment