Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 29, 2014

TAMTHILIA: SIRI YA MTUNGI SEHEMU YA 15 & 16 ITAZAME HAPA

SEHEMU YA 15: 
Cheche anakutana na maamuzi magumu sana toka kwa “mmiliki” mpya wa studio ya Mtungi. Shalima hato salimu amri. Inaonekana Cheche amekamatika kwa Shalima na kua mwenza katika biashara. Kwa upande wa mke wake, Cheusi, umekua muda mwafaka wa kulipwa kwa mabaya yote, amechoshwa na hali ya mumewe kuto kua mwaminif., Siku alipo kutana na mwanamke asie na aibu Lulu, Cheche alikua mpole sana na kusinyaa. Anaamua kuondoka na kuamua kuanza kufanya mambo yake mwenyewe kwa ajili ya kupta mabadiliko. Na kumwacha Cheche ajikomboe mwenyewe. Ufufuko wa Nusura kwa mpenzi wake wa zamani Duma unaibua penzi jipya linalo mfanya Duma kumng’ang’ania Nusura na kutotaka kumwacha anajiweka karibu na kumsahau mdogo wake Stephen na kumfanya anajikita na maisha ya kiovu.
SEHEMU YA 16: 
Duma anajipatia kipato kidogo sana kwa kazi yake ya DJ kwenye Hoteli ya hali ya chini sana, anagombana na utawala wa Hoteli na kuamua kujiingiza kwenye shughuli ya kutafuta pesa za haraka. Anajingiza kwenye biashara ya madawa ya Kulevya akishirikiana na Golden. Mpaka wa maadili unasogezwa mbali zaidi baada ya Duma kumfanya mdogo wake aige vitendo viovu. Nusura anakimbia unyanyaswaji wa nyumbani kwa Mzee Kizito na kuamua kwenda Nyumbani kwa mama yake Sophia. Huko anapata hamasa ya ajabu toka kwa binti jirani yao mwenye akili na shujaa jinsi alivyo ishi na mwanae. Wakati huo huo Cheche anapata kazi ya nje ya kurekodi video ya siku ya Ngoma zakumtoa mwali yeye na “msaidizi” wake Shoti wanakumbwa na balaa baada ya kumvamia binti mdogo na wapekee wa Big mama.

No comments:

Post a Comment