Wananchi wakishirikiana kuondoa mawe barabarani ili kuruhusu
magari kuendelea na safari zake. JESHI la Polisi jijini Dar limelazimika
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa
jina la Machinga waliokuwa wanaandamana kuelekea ofisi za jiji eneo la Kamata,
Kariakoo jijini Dar es Salaam Jana.
Machinga hao waliamua kuchoma matairi na kuweka mawe
barabarani wakati wa maandamano hayo ambapo madai yao ni kuhusu unyanyasaji
wanaofanyiwa na askari wa jiji ikiwemo kunyang'anywa mali zao.chanzo GPL
No comments:
Post a Comment