Mlinzi wa klabu ya Barcelona Thomas amefanyiwa tiba ya upasuaji wa tatizo lake la misuli lililokuwa linamsumbua kwa muda mrefu tangu akiwa klabu ya Arsenal.
Nahodha huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal aliyesajiliwa na klabu ya Barcelona kwenye usajili wake wa dirisha ya majira ya joto alisaini mkataba na klabu ya Barcelona utakao muweka klabuni hapo mpaka mwaka 2019 lakini mpaka sasa hajaitumikia timu hiyo kwenye mchezo wowote ule.
“Upasuaji umefanyika nchini Finland na Daktari Sakari Orava na taarifa za kitabibu zinasema kuwa itamchukua hadi miezi minne kurejea mchezoni," taarifa ya klabu ya Barcelona ilisema.
Daktari Sakari Orava raia wa Finland aliyemfanyia upasuaji Thomas Vermaelen ndiye aliyemfanyia upasuaji meneja wa sasa wa klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola, miaka 16 iliyopita alipokuwa akisumbuliwa na maumivu sugu ya misuli wakati akikipiga kwenye klabu ya Barcelona.
No comments:
Post a Comment