.jpg?width=650)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dr. Finella Mukangara (katikati) Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Abdilah Jihadi Hassan (kulia) wakiwa na Mwandishi wa Habari Salim Said Salim na Mama Fatma Karume wakiwa katika Hafla ya utoaji wa tunzo kwa wanamichezo bora kwa mwaka 2013/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
.jpg?width=650)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi tunzo ya Heshma Mama Fatma Karume mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Karume tunzo hiyo imetelolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa kutambua mchango mkubwa wa Mzee Karume kwenye michezo, ikiwa ni pamoja na kujenga majengo ya klabu za Yanga na Simba na mambo mengine mengi.
.jpg?width=650)
.jpg?width=650)
.jpg?width=650)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipomkabidhi Tunzo Mwanamichezo bora wa jumla wa Mwaka Sheridah Boniface wakati utoaji wa tunzo zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Taswa katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam (kushoto)Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari za Michezo TASWA Bw.Juma Pinto.
.jpg?width=650)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bara Dr. Finella Mukangara ,Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Abdilah Jihadi Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo waliopta tunzo zilizotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo katika ukumbi Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment