Bibi Mariam Abdallah, mwenye umrin wa miaka 60, mkazi wa Kijiji cha Mnanila, ambaye anadaiwa kushushiwa kipigo nyumbani kwake na Askari wa JWTZ,akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni kwa matibabu.
Inadaiwa kuwa Novemba 23 mwaka huu, majira ya saa tatu usiku, watu wanne waliokuwa wamevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), walivamia nyumbani kwa bibi huyo wakimtafuta msichana aliyejulikana kwa jina moja la Editha, ambaye anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa wanajeshi hao.
Hata hivyo bibi huyo aliwajibu kuwa hakuwa anamfahamu msichana huyo na kwamba yeye hana mtoto wa kike, lakini cha kushangaza mmoja wa askari jeshi hao alianza kumshushia kipigo mfululizo kwa mateke na ngumi na kumjeruhi sehemu mbali mbali za mwili wake hasa maeneo ya usoni na kumsababishia maumivu makali kiasi cha kulazwa hospitali.
Credit kigomalive
No comments:
Post a Comment