Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, January 16, 2015

ASKARI HAWA GETINI AIRPORT WANAKAGUA NINI KWENYE MABEGI YA WANAOTOKA UWANJANI?

Askari Polisi akikagua katika begi la mmoja kati ya watu wanaotoka ndani ya uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo ambapo askari hao wamesimama usawa wa geti la kutokea magari na kusimamisha baadhi ya magari na kisha kukagua mabegi kama hivi, jambo ambalo limelalamikiwa na baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakisumbuliwa na askari hao ambao wamekuwa wakichagua baadhi ya magari ya kuyakagua kama hivi.
Askari huyo akihamaki kupigwa picha.
Akifurahia ukodaki baada ya kugundua amepigwa picha huku akirejesha begi hilo garini baads ya kuhakiki alichokuwa akihisi kuwa hakuna.
CREDIT:SUFIANIMAFOTO

1 comment:

  1. Acha kupotosha watanzania hilo ni geti la kuingia na wala sio la kutokea. Hao askari wanafanya initial check up security

    ReplyDelete