Unadhani simu yako ya mkononi ni kichaka kikubwa kinachoweza kuhifadhi siri zako zote?
Jibu ni hapana. Kwani teknolojia inamwezesha
mtumiaji yeyote kuingilia mawasiliano katika simu yako na kufyonza
taarifa mbalimbali kama ujumbe mfupi, barua pepe, simu zinazotoka na
kuingia, picha unazopiga au kutumiwa hata video, pia inaweza kubaini
eneo alipo mtu.
Kwa lugha nyepesi kitendo hiki huitwa udukuzi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Profesa John Nkoma anafafanua udukuzi akieleza kuwa ni matumizi
ya teknolojia inayowezesha kuingilia mawasiliano ya mtu katika simu au
kifaa chochote cha mawasiliano.
Udukuzi wa Serikali
Novemba mwaka jana, Kampuni ya Kimataifa ya Simu
za Mkononi ya Vodafone, ilitoa taarifa
inayoonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeweka nyaya za siri katika mtandao wa Vodacom na kunasa mawasiliano ya wateja 98,765 kwa mwaka 2013.
inayoonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeweka nyaya za siri katika mtandao wa Vodacom na kunasa mawasiliano ya wateja 98,765 kwa mwaka 2013.
Katika ripoti hiyo,(Law Disclosure Enforcement),
Tanzania inatajwa kuwa ni nchi ya pili duniani miongoni mwa nchi 29
ambazo Vodafone inatoa huduma ikiwa nyuma ya Italia kwa kufuatilia,
kuingilia au kunasa mawasiliano ya simu.
Italia inashika nafasi ya kwanza kwa mawasiliano 605,601 ya raia wake kufuatiliwa na taasisi za kiusalama za Serikali.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, Januari Makamba alidai kushtushwa na taarifa za Serikali
kunak-ili mawasiliano ya simu kwa kutumia nyaya za siri.
“Hata mimi imenishtua kidogo kwa sababu sheria za
usalama za mawasiliano, kunakili chochote kunafanyika kwa sheria tu,”
anasema.
Hata hivyo, Makamba anakiri kuwa Serikali kupitia taasisi za usalama hulazimika kuomba taarifa za wateja kwa ajili ya uchunguzi.
- Mwananchi
No comments:
Post a Comment