Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 28, 2015

Kasisi wa kwanza mwanamke aapishwa UK

Libby Lane kuwa kasisi wa kwanza mwanamke
Kanisa moja nchini Uingereza jana limemuapisha mwanamke wa kwanza kuwa kasisi.
Mchungaji Libby Lane kama anavyojulikana sasa atakuwa kasisi wa Stockport katika sherehe iliofanyika katika eneo la York Minster,ikiwa ni miezi sita tu baada ya kanisa hilo kumpigia kura ili kumaliza utamaduni wake wa wanaume kuwa makasisi.


Kasisi huyo amesema kuwa iwapo uchaguzi wake utawafanya wanawake kubaini uwezo wao basi anafurahia.

Hatua hiyo imeendelea kuzua hisia tofauti miongoni mwa wafuasi wa kanisa hilo la kianglikana duniani.chanzo BBC

No comments:

Post a Comment