Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Uzini na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha mapinduzi Mh. Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Dunga wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2010, Katika mikutano mbalimbali ambayo Kinana amekuwa akihutubia na kuzungumza na wananchi na wana CCM amekuwa akihimiza viongozi kufuata maadili ya uongozi jambo ambalo ni muhimu na la lazima katika uongozi ili kuutumikia umma katika misingi mizuri na yenye tija,Katika ziara hiyo Kinana amewahimiza Wazanzibari kuipigia kura ya ndiyo Katiba mpya iliyopendekezwa kwakuwa inatatua kero nyingi za wanzanzibari katika muungano na kuwafanya wawe na uhuru zaidi , kama vile Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iwapo Rais wa Jamhuri atatoka Bara, Zazibar kujiunga na jumuiya za kimataifa bila kikwazo, kuwa na uhuru wa kukopa na mambo mengine mengi yaliyomo katika katiba hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UZINI-ZANZIBAR)
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakati alipowasili katika kijiji cha Dunga jimbo la Uzini mkoa wa Unguja Kusini leo.
No comments:
Post a Comment