Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, January 30, 2015

Malaysia yasitisha msako wa MH370



MH370 ndege ya Malaysia iliyopotea ikiwa njiani kutoka Malaysia kuelekea China
 Serikali ya Malaysia imesitisha shughuli ya kuitafuta ndege ya iliyopotea ya MH370 na kuitaja kama ajali huku ikisema hapakuwa na manusura wa ajali hio.
 Hapajawi kuoenekana dalili ya ndege hiyo iliyopotea ikiwa safarini kuelekea China kutoka Malaysia tarehe 8 mwezi Machi mwaka 2014,
 Maafisa wakuu wanasema shughuli ya kuipata ndege 
 
hiyo, bado inaendelea lakini inasemekana abiria 239 waliokuwa kwenye ndege hio walifariki.
 Ndege hiyo bado haijulikani iliko na wala kujulikana ilikopotelea licha ya shughuli kubwa ya kimataifa kuitafuta ksuini mwa bara hindi.
 Tangazo la serikali ya Malaysia, Alhamisi, inatoa fursa kwa jamaa wa waathiriwa wa ajali hio kulipwa fidia.
 Maafisa waliongeza kusema kwamba serikali bado imeipa kipaombele shughuli ya kuitafuta ndege hio na kwamba imefanya kila iwezalo angalu kupata dalili ya ikokwenda.
 Vyombo vinne vya baharini vilivyokuwa vinafanya msako baharini kwa kutumia teknolojia ya kisasa 'Sonar' kutafuta angalau mabaki ya ndege hio vimesitisha shughuli hio.
 Kulingana na picha za Satelite, mabaki ya ndege hiyo huenda yako katika ufuo wa mji wa Perth Magharibi mwa Australia.

No comments:

Post a Comment