Jasusi wa nchini Cuba aliyeachiwa na Marekani hivi karibuni
hivi sasa amekuwa Baba baada ya ombi lake la kutaka mbegu zake za kiume
zikapandikizwe kwa mkewe wakati alipokuwa jela.
Mbegu za Gerardo Hernandez zilisafirishwa kwenda Cuba
alikokuwa mkewe.Hernandez alikua akitumikia kifungo nchini Marekani kwa makosa
ya kufanya vitendo vya kijasusi, lakini aliachiwa mwaka jana yakiwa ni matunda
ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Cuba.
Cuba na Marekani zilitangaza mwezi Desemba kuwa nchi hizo
zimerejesha uhusiano wa kidiplomasia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1961.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment