Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 11, 2015

Mliberia Yanga SC aibiwa hotelini na Mrembo, Alimuacha Chumbani Akaenda Mazoezini, Akabeba Simu na Laptop


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Kpah Sherman
Na Imelda Mtema
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Kpah Sherman, amekumbana na mkasa wa aina yake ambao unaweza kuuita “karibu Dar es Salaam” baada ya kuibiwa vitu vyake vya thamani.
Sherman, raia wa Liberia, ameibiwa vitu mbalimbali vya thamani na mrembo mmoja raia wa Tanzania.
Mshambuliaji huyo alikuwa na uhusiano na mrembo huyo aliyejulikana kwa jina moja la Cynthia ambaye inaelezwa walilala pamoja na asubuhi Mliberia huyo akaondoka kwenda mazoezini.
Kitendo cha kuondoka kwenda mazoezini ndicho kilitoa nafasi kwa mrembo huyo kuamua kuondoka na simu na saa yake ya thamani pamoja na laptop.“Unajua hoteli yetu ina self (kifaa maalum cha kuhifadhia vitu vya thamani). Sasa Sherman aliweka fedha zake mule ndiyo ikawa nafuu yake.
“Lakini kweli mrembo huyo kafanya jambo ambalo si la kiungwana na ametudhalilisha Watanzania,” 



alisema meneja wa hoteli hiyo ya kisasa akiomba chonde isitajwe jina hasa baada ya kujua Championi lina mkasa mzima.
Juhudi za kumhoji Sherman kuhusiana na hilo zimekuwa na ugumu baada ya kuonekana hataki kulizungumzia wakati akiwa Zanzibar anaitumikia Yanga kwenye michuano ya Mapinduzi ambayo waling’olewa juzi.
hanzo hicho kilizidi kueleza kuwa baada ya msichana huyo kuondoka, kila alipopigwa simu na Sherman, hakupokea.Baadaye alipokea na kuanza kumtishia Sherman kuwa atamshtaki huku akimpa vitisho kuwa yeye siyo raia wa Tanzania.
Gazeti hili lilimtafuta msichana huyo kwa njia ya simu ambapo alisema kuwa alifanya vile kwa kuwa alikuwa akimdai huyo Mliberia Sh 500,000 alizomkopa wakiwa nchini Thailand.
“Mimi ninafahamiana naye siku nyingi sana, namdai yeye na wakala wake tangu tulipokutana Thailand, sitatoa kitu na nimemueleza,” alisema na baadaye taarifa hiyo ikatiliwa mkazo na mtu aliyejitambulisha ni mama wa msichana huyo.
“Ni kweli anamdai, tena wakala wake ndiye alisababisha yote hayo.”
Taarifa za mwisho wakati tunakwenda mitamboni zinaeleza, tayari kesi imefunguliwa katika kituo kimoja cha polisi lakini Sherman kukosa muda wa kutosha na hoteli kuhofia kuchafua jina lake, vimekuwa vikikwamisha kuifuatilia.

No comments:

Post a Comment