Wasamalia wema wakifanya utaratibu wa kumuokoa Dereva wa Gari aina ya Isuzu Trooper iliyopiga mweleka katika makutano ya Shule ya Msingi Oysterbay,mara baada ya kugongana na gari nyingine aina ya Toyota Vitz iliyokuwa ikitokea upande wa Coco Beach jijini Dar mchana wa leo na kupekea dereva wa Gari hii (alikuwa ni Mama mtu mzima ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) kuumia sehemu ya kiuno na mkono.Gari hii ilikuwa inatokea upande wa St. Peter's kuelekea Morogoro Store na Vitz ilikuwa ikitokea upande wa bahari na kuvuka ghafla barabara hiyo. Picha zote kwa hisani ya Michuzi BlogMashuhuda wakiwa wameizunguka gari hiyo mara baada ya kufanikiwa kumtoa Mama aliekuwa akiendesha Gari hilo.
Huyu ndio Mama aliekuwa akiendesha Gari iliyopinduka.Picha na Mdau Pius Micky.
No comments:
Post a Comment