Na Gabriel Ng’osha/Risasi Mchanganyiko
KICHANGA kinachokadiriwa kuwa na umri wa miezi nane, wiki
iliyopita kiliiokoa familia yake kuteketea kwa moto, baada ya kuamka usiku na
kulilia kunyonya, kitendo kilichomshtua mama yake aliyebaini nyumba yao ilikuwa
ikiungua, huko Kibamba Lungwe jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya nyumba iliyoungua.
Akisimulia tukio hilo, mama wa kichanga hicho, Asha Mohamed,
alisema alishtuka baada ya mtoto kuanza kulia akitaka kunyonya, alipoamka ndipo
akaona mwanga mkali juu ya paa, hali iliyomlazimu kuamka na kwenda kumgongea
Abuu ili kutafuta njia ya kutoka,” alisema mama huyo akiongeza kuwa sebuleni, moto
ulikuwa umetapakaa.
Kijana Abuu Masoud (15), baada ya kuamshwa, alionyesha
ujasiri na upendo mkubwa kwa kujitoa mhanga kuwasaidia wadogo zake watatu
waliokuwa wamelala katika moja ya vyumba vya nyumba hiyo.
Baada ya kuingia katika chumba hicho, alifanikiwa kumtoa
mtoto mmoja.
Watoto walionusulika kuteketea kwa moto.
“Nilipofungua mlango wa sebuleni nikaona moto na moshi
mwingi sana, roho iliniuma sana kwani chumba cha pili kulikuwa na wadogo zangu
watatu wamelala, nikaamua kuvaa ujasiri
na kujitosa katika chumba kile na
kufanikiwa kutoka na mtoto mmoja, wakabaki wawili,
baada ya kurudi ndani nikapata wazo la kuzima Mean switch,
nilipoenda kuishika ikaniangukia kichwani kwani ilikuwa imeshaungua, ndiyo
nikaungua na kushindwa kuwatoa waliobakia, ingawa baadaye kuna msamaria mwema
mmoja alijitokeza na kuja kubomoa mlango na kuwatoa wengine,” alisema kijana
huyo.
..Kitanda walichokuwa wamelala.
Mama wa mtoto mchanga alifanikiwa kutoka pasipo kudhurika.
Aidha baba mwenye nyumba hiyo, Khalfani Maketemo, ambaye
wakati nyumba yake inaungua yeye na mkewe walikuwa hospitali alikokuwa
amelazwa, anadai chanzo cha moto huo ni shoti iliyoanzia kwenye bati na
anaamini ni kutokana na kuunganishwa
vibaya kwa waya unaopitisha umeme kutoka kwenye nguzo kwenda kwenye nyumba.
Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya majirani walisema;
“Uunganishwaji wa umeme ni wa kubabaisha, waya unagusana na bati jambo ambalo ni hatari kama waya utachubuka na mvua
kunyesha’’.Familia hiyo kwa sasa haina sehemu ya kujisitiri nyumba nzima
imeteketea.CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment