Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 10, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA - DIRISHA DOGO LA USAJILI


Real Madrid wamewasiliana kwa mara ya kwanza na kipa wa Manchester United David De Gea, kutaka amrithi Iker Casillas. Huenda Real wakatoa pauni milioni 30 (Daily Mirror), Manchester United watampa David De Gea mshahara wa pauni 140,000 kwa wiki ili asishawishike kwenda Real (Daily Star), beki wa Southampton Nathaniel Clyne, 23, ananyatiwa na Manchester United (Daily Mirror), mshambuliaji wa Arsenal Yaya Sanogo, 21, anajiandaa kwenda Crystal Palace kwa mkopo, akikataa kwenda Hull City (Metro), Liverpool wanafikiria kumruhusu kiungo Lucas, 28, kwenda Inter Milan, huku klabu hiyo ya Italy ikitaka kutoa pauni milioni 7 kumnunua (Daily Mirror), Tottenham inamnyatia mashambuliaji wa Juventus Sebastian Giovinco, 27, (Fichajes.net) 

Sunderland watamruhusu mshambuliaji wao Jozy Altidore, 25, kurejea Marekani mwezi huu, huku timu tatu za MLS zikimtaka (Guardian).- leo kimya kidogo- Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Uhamisho uliotjibitishwa nitakufahamisha utakapothibitishwa

No comments:

Post a Comment