Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 12, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA- DIRISHA DOGO LA USAJILI

Liverpool huenda wakamuuza mshambuliaji wao Mario Balotelli, 24, mwezi huu ili kupata fedha za kumnunua Gonzalo Higuain, 27 kutoka Napoli na kipa wa Sampdoria Sergio Romero, 27 (Daily Express), Kiungo wa Newcastle Moussa Sissoko, 25, huenda akaondoka St James Park baada ya kukaririwa akisema "Ni matumaini yangu siku moja nitakwenda timu kubwa". Arsenal wameripotiwa kumnyatia mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ufaransa (Newcastle Chronicle), Manchester United wanajaribu kumsajili beki wa kati Aymeric Laporte kutoka Atletico Bilbao kwa pauni milioni 25 (Daily Star), 
mshambuliaji wa Newcastle Papiss Cisse, 29, anaandaliwa kuziba nafasi ya Wilfried Bony anayeondoka Swansea kwenda Manchester City (Sun), Aston Villa wanajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Valencia Cares Gill, 22 kwa pauni milioni 3.2 ili kumaliza ukame wa magoli (Daily Mirror), West Brom na Crystal Palace wanataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Rickie Lambert, 32, mara baada ya Divock Origi, 19, kurejea kutoka Lille anapocheza kwa mkopo (Daily Mirror), Liverpool wanakaribia kumuuza winga wao Oussama Assaidi kwenda Al-Ahli ya Dubai kwa pauni milioni 4.7 (Daily Mirror), mshambuliaji mkongwe kutoka Cameroon anayechezea Everton, Samuel Eto'o, 33, huenda akahamia Sampdoria ya Italy kwa mkopo wa miezi 18 (Liverpool Echo), 


Arsenal na Manchester United wanataka kumsajili beki wa kati Virgil van Gijk, 23 kutoka Celtic (Daily Star), Wolverhampton wamekubaliana ada ya uhamisho kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Benik Afobe, 21 kutoka Arsenal (Express na Star). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Habari zilizothibitishwa za usajili nitakujulisha mara zitakapodhibitishwa.na Salim Kikeke

No comments:

Post a Comment