Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 11, 2015

TETESI ZA SOKA ULAYA::SWANSEA WAKUBALIANA NA MAN CITY KUHUSU BONY

Swansea City wamekubali ada ya uhamisho ya takriban pauni milioni 30 kutoka kwa Manchester City ya kumnunua Wilfried Bony, 26.
Meneja wa Swansea, Gary Monk alisema kuwa itahitaji "kitita cha ajabu" kumhamisha Bony kutoka Swansea.
Alikuwa mfungaji bora wa mwaka wa kalenda 2014 akipachika mabao 20.
Bony alijiunga na Swansea mwaka 2013 akitokea Vitese Arnhem kwa pauni milioni 12.
Mchezaji huyo alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 90 kwenye mechi dhidi ya QPR siku ya mwaka mpya.

Bony kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

No comments:

Post a Comment