Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 14, 2015

UKATILI::KICHANGA AUAWA, ATIWA KWENYE MFUKO WA RAMBO


Mwili wa kitoto kichanga uliotupwa kwenye jalala.
Stori: Mwandishi Wetu, Mbeya/UWAZI UKATILI, Mtoto mchanga ambaye anasadikika kuwa wa siku saba, amekutwa akiwa ameuawa na mwili wake kuwekwa kwenye mfuko wa rambo kisha kutupwa pembeni mwa jalala. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Mtaa wa Kaloleni  katika Mji wa Tunduma katika Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya .
Wakizungumza na gazeti hili mashuhuda ambao hawakupenda majina yao kuandikwa gazetini walisema kuwa walimkuta mtoto huyo akiwa amenyongwa kisha kuwekwa kwenye karatasi ya naironi (rambo) .
Waliongeza kuwa mtoto huyo alitambulika baada ya watoto wadogo wakiwa katika michezo yao katika maeneo yao kuuona mfuko huo wa rambo na kuufungua  ndipo wakatoa taarifa wa wazazi wao,” alisema mmoja wa wazazi wa eneo hilo.
Msemaji wa jeshi la Polisi mkoani Mbeya, SACP Ahmed Msangi.
“Hiki kitendo ni kibaya sana na aliyefanya unyama huu anastahili adhabu kali. Huwezi kulea mimba miezi tisa kisha unamza mtoto na kumnyonga shingo hadi kufa, ni ukatili uliokithiri, tena mtoto huyu ni kama wa siku saba, hii ni kwa sababu kitovu chake kilionesha dalili za kupona,” aliongeza.
Hata hivyo, aliyefanya kitendo hicho cha kikatili 



hakuweza kutambulika mara moja.
Wakithibitisha habari hiyo, kiongozi mmoja wa polisi katika kituo kidogo cha Tunduma alisema ni kweli kimetokea na mwili huo wa mtoto huyo umepelekwa katika hospitali ya serikali iliyopo mjini hapa kwa ajili ya uchunguzi.
“Tunaomba wenye kujua aliyefanya haya atuletee jina ili tumkamate,” alisema ofisa huyo bila kutaja jina lake kwa kuwa siyo msemaji wa polisi. Msemaji wa jeshi hilo mkoani Mbeya ni SACP Ahmed Msangi (pichani).

No comments:

Post a Comment