DUNIA inazidi kwenda kubaya! Mwanaume aliyejulikana kwa jina
la Maulid Mussa (35), mkazi wa Kijiji cha Igoko wilayani Uyuwi, Tabora
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa madai ya kumuua mkewe, Zuhura Juma (31) kwa
kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa tisa usiku wa
kuamkia Jumatatu ya Januari 12, mwaka huu katika Kijiji cha Usagala Kata ya
Magengati Tarafa ya Puge wilayani Nzega, Tabora nyumbani kwa wazazi wa mwanamke
huyo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Maulid alifikia uamuzi huo mgumu
baada ya mkewe kumuuliza habari alizozisikia kuwa aliuza shamba la tumbaku la
familia bila yeye kujua hali ambayo haikumpendeza mwanaume huyo.
Bw. Maulid Mussa (35) anayetuhumiwa kumuua mkewe na
kujichoma kisu mwenyewe. UWAZI LAFUATILIA TUKIO
Baada ya taarifa hizo kutua kwenye dawati la gazeti hili,
mwanahabari wetu alifika kwenye kijiji hicho ili kupata maelezo ya kina kutoka
kwa mashuhuda wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa shuhuda, siku moja kabla ya tukio, Maulid
alimfuata marehemu kwa wazazi wake alipokimbilia baada ya mzozo wa shamba
akimtaka arudi nyumbani kuendelea na maisha.
Alipofika, alimkuta mkewe na watoto wao wanne wakila.
Alikaribishwa chakula cha mchana, akajumuika.
Siku iliyofuata alimweleza mkewe sababu ya yeye kumfuata ni
kutaka arejee nyumbani, lakini mke alikataa kwa vile wazazi wake walikuwa nje
ya kijiji hicho.
MUME AWAFUATA WAZAZI
“Baada ya Maulid kupewa maelezo hayo, alichukua uamuzi wa
kuwafuata wakwe zake katika Kijiji cha Busondo ambacho ni jirani na kijiji
hicho, akawaeleza lengo la safari yake ambapo wakwe hao walimwambia arudi
kijijini akawasubiri.”
Wazee na vijana wakiomboleza msibani. ALA CHAKULA CHA MWISHO
NA FAMILIA
“Maulid alirudi katika kijiji cha wakwe zake. Ilikuwa jioni,
akamkuta mkewe ameandaa chakula cha jioni, walikula wote na watoto wao kisha
akaaga kwa furaha kwamba anarudi nyumbani kwake,” alisema shuhuda mmoja akiomba
jina lake kusitiriwa.
MTOTO WA KAKA WA MAREHEMU ASIMULIA
Shuhuda mwingine wa tukio hilo ni mtoto wa kaka wa marehemu
ambaye naye aliomba jina lake kutoandikwa gazetini, yeye alisema:
“Usiku wa tukio nilisikia sauti ya mtoto akilia kuashiria
kuna tatizo, nikaamka na kutoka nje ili kujua kuna tatazo gani.
“Nilipofika nje niliona baiskeli ya mume wa marehemu ikiwa
imeegeshwa kwenye nyumba aliyolala. Sikuwa na wasiwasi.
Waombolezaji wakiwa kaburini mara baada ya kumzika marehemu
Zuhura Juma. “Lakini muda mfupi baada ya kurudi ndani nilisikia sauti ya
mwanamke akiomba msaada eneo la nyuma ya nyumba aliyolala marehemu. Alikuwa
akisema, ‘jamani nauawa, naomba mnisaidie nakufa! Nakufa!’ Nikatoka nje na
kwenda ilikokuwa ikitokea sauti. Nilishtuka kumkuta Zuhura amelala chini huku
akiwa ametapakaa damu na majeraha mgongoni na shingoni. “Nilipiga kelele kuomba
msaada, watu wakaja. Ndipo tukaanza kumfuatilia Maulid kwani niliwaambia niliiona
baiskeli yake nje ya nyumba.
“Tulimkuta Maulidi kichakani naye akiwa ametapakaa damu.
Kumbe alijaribu kujichinja mwenyewe shingoni kwa lengo la kujimaliza baada ya
zoezi la kujiua kwa kunywa sumu kushindikana ambapo alitapika.”
BABA WA MAREHEMU
Naye baba wa marehemu Zuhura, Juma Ramadhani alipozungumza
na Uwazi kuhusu mauaji ya mwanaye alisema:
Marehemu Zuhura Juma enzi za uhai wake. “Kusema ukweli
maumivu niliyoyapata kwa kuuawa mtoto wangu tena kikatili vile siwezi kuyatolea
mfano. Mimi nachukulia mauaji haya kama kuidhalilisha familia yangu. Naiomba
serikali itende haki kwa kutoa hukumu na adhabu kali kwa Maulid ili iwe
fundisho kwa wanaume wenye tabia ya kufanya ukatili kwa wake zao.”
MWENYEKITI WA KIJIJI
Mwenyekiti wa Kijiji cha Usagali, Ally Said Mlenda
alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na aliyapokea kwa masikitiko makubwa.
No comments:
Post a Comment