Vitu vya kumbukumbu vya aliyekuwa rais wa 16 wa Marekani
Abraham Lincoln vimeuzwa katika mnada mjini Dallas nchini Marekani na kupata
dola 800,000.
Msokoto mmoja wa nywele za rais huyo aliyeuawa umeuzwa kwa
dola 25,000 lakini barua iliokiri kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe havikuwa
vizuri haikuuzwa.
Barua iliotiwa sahihi na naibu wake John Wlkes Booth iliuzwa
kwa dola 30,000 huku agizo lake la kijeshi likitia kibindoni dola 21,250.
Vitu vya Lincoln vilipigwa mnada mjini Dallas marekani
Ukusanyaji wa vitu hivyo 300 ulianzishwa mwaka 1963 na
mmiliki wa jumba la sanaa Donald Dow aliyefariki miaka mitano iliopita.
Mwanawe Greg amesema kuwa ni wakati wakusanyaji wengine
wapate fursa ya kuifurahia.
Amesema kuwa babaake alikuwa ameanza ukusanyaji huo kutokana
na maslahi yake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na historia ya
kijeshi,lakini baadaye alikuwa na hamu na Lincoln na mauaji yake.
No comments:
Post a Comment