KAMATI
ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), imekiri kuwa hadi sasa
Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ipo, lakini pamoja na
kusainiwa na Rais bado haijaanza kutekelezwa jambo linalosababisha
misamaha ya kodi izidi kupaa.
Aidha,
Zitto alimwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
awasiliane na Serikali ili kubaini chanzo na sababu zinazofanya sheria
hiyo hadi sasa haitangazwi kwenye gazeti la Serikali na kutekelezwa kwa
mujibu wa Sheria
Hayo
yalibainishwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kabwe
Zitto, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Ikulu
kushangazwa na kamati hiyo kuendelea kulalamikia misamaha ya kodi,
wakati wameshindwa kupitisha muswada wa Sheria utakaosaidia kufuta
misamaha ya kodi nchini.
“Si
kweli kwamba hatujapitisha sheria, Mkurugenzi wa Ikulu aangalie taarifa
zake vizuri, Sheria hii tayari imepitishwa ila mpaka sasa
haijatekelezwa na ndio maana madhara ya misamaha ya kodi inazidi
kuendelea,” alisisitiza Zitto.
Alisema
baada ya kupokea taarifa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu
kuzidi kupanda kwa misamaha ya kodi ambayo imefikia kiasi cha Sh
trilioni 1.82 kwa mwaka wa fedha 2013/2014, kamati hiyo ilimuagiza
Waziri wa Fedha kuitangaza Sheria hiyo kwenye gazeti la Serikali ili
iweze kutekelezwa.
Alisema
pamoja na kwamba Sheria hiyo awali ilikuwa na mapendekezo makubwa
ambayo yangewezesha tatizo la misamaha ya kodi nchini kuwa historia,
ilipopitiwa na Kamati ya Bunge ya Bajeti, mapendekezo hayo yalipunguzwa
ili kuwezesha misamaha ya kodi kuzidi kuendelea nchini.
“Hili
ndio tatizo kubwa tulilonalo sasa, sisi Kamati ya PAC tunataka na
tunapendekeza na kila siku tunasisitiza juu ya kuondolewa kwa misamaha
hii ya kodi, lakini wenzetu wa Kamati ya Bajeti hawataki wanataka
misamaha ya kodi iendelee,” alisema.
Hata
hivyo, alibainisha kuwa Sheria hiyo ya VAT iliyotakiwa kutekelezwa
tangu Januari mwaka huu, ina wigo mkubwa wa kupunguza tatizo hilo la
misamaha ya kodi endapo haitaendelea kukaliwa na Serikali.
No comments:
Post a Comment