Raia wa Uingereza aliyewadhalilisha kingono watoto wa kiume
katika mji mdogo wa Gilgil nchini Kenya anatarajiwa kuhukumiwa leo nchini
Uingereza.
Hii ni baada ya Mahakama ya Birmingham kumkuta na hatia ya
kuwadhalilisha watoto wa kiume kingono na pia kupatikana na picha za utupu za
watoto.
Simon Harris mwenye umri wa miaka 55 ambaye alikuwa
akiendesha Mradi wa misaada kwa Jamii anaaminika kufanya maovu hayo kwa karibu
miaka ishirini.
Gladys Njoroge amekutana na baadhi ya waathirika ambao
waliomba majina yao yahifadhiwe.
No comments:
Post a Comment