Bw. Mugusuhi Nyarusahe (39) aliyecharangwa kwa visu na
wenzake.Stori:Gregory Nyankaira, Butiama/Risasi Mchanganyiko
MTU mmoja, Mugusuhi Nyarusahe (39) mkazi wa Kijiji cha
Kinyambwiga wilayani Bunda, amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU),
cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara baada ya kucharangwa visu na wenzake
tumboni, katika kile
kilichodaiwa kuwa ni mzozo wa mgawo wa fedha zilizotokana
na mauzo ya ng’ombe, tukio lililotokea wiki iliyopita. Nyarusahe ambaye ni
maarufu kwa jina la Serikali, alipatwa na mkasa huo baada ya kuzuka ugomvi
katika baa moja iitwayo Gateway Bar & Guest House iliyopo Kiabakari
wilayani Butiama.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kundi la watu sita lilifika
katika baa hiyo na kujitenga kando mishale ya saa 11 jioni na kuanza kuagiza
vinywaji huku wakiwa na mazungumzo yao.
Ghafla, watu hao walianza kumwagiana pombe ovyo vichwani na
kuzua taharuki kubwa kwa wateja wengine huku wakipasua chupa za bia na Mukebha
Marwa alichomoa kisu kutoka ndani ya koti alilokua amevaa na kumchoma Mugusuhi
na kusababisha utumbo kumwagika chini.
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema watu hao walikuwa
wakibishana juu ya mgawo wa fedha zilizotokana na mauzo ya ng’ombe
wanaosadikika kuwa wa wizi.
Akizungumza akiwa hospitalini, Mugusuhi alisema ameanza
kujitambua baada ya kuzirai tangu alipochomwa kisu na kwamba baada ya kukatwa
utumbo mara tatu na kushonwa ameanza kupata nafuu “Mungu atanisaidia nitapona,”
alisema.
Jeshi la polisi kupitia kwa msemaji wake Kamanda ASP Alex
Kalangi limethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa hakuna mtu
aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment