Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, February 13, 2015

KOVA APIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA VIJANA WA CUF

 Kamishna Kova akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
Wanahabari wakimsikiliza Kamishna Kova (hayupo pichani)

KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar e s Salaam, Suleiman Kova  ametoa tamko mbele ya wanahabari juu ya maandamano ya vijana wa Chama cha Wananchi CUF (JUVICUF) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Leo.

Kamanda Kova amewataka vijana wa CUF  kutoandamana  leo na kama wataandamana jeshi hilo halitakuwa tayari kuona maandamano hayo yakifanyika .

Alisema kuwa maandamano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika leo Februari 13 mwaka huu


   kutoka  Buguruni, Shule ya Uhuru, Mnazi Mmoja, Mtaa wa Ohio hadi Tume ya Taifa ya Uchaguzi  na kisha Wizara ya Mambo ya Ndani ,kwa dhumuni la kuitaka Tume ya Taifa ya Uchanguzi (NEC) iongeze siku za uandikishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutoka siku saba hadi siku 14, pamoja na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi nchini.

Kova ametaja sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa siku waliyoomba ni siku ya kazi, ambapo maandamano hayo yakifanyika yatasumbua mfumo mzima wa shughuli za jiji zima, kibiashara, huduma za afya, walemavu, watoto na n.k.


(Habari/Picha:  Gabriel Ng’osha/GPL)

No comments:

Post a Comment