Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, February 17, 2015

Lowassa, Membe huru ndani ya saa 24


Dar es Salaam.  Kifungo cha miezi 12 walichopewa makada sita wa CCM kwa kukiuka kanuni na taratibu za chama hicho na kuanza kampeni za kuwania urais kabla ya wakati, kinamalizika ndani ya saa 24 na hatma yao kusubiri tathimini itakayofanywa na kamati ndogo ya maadili ili kubaini iwapo walitekeleza ipasavyo adhabu hiyo au la.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alithibitisha jana kuwa muda wa adhabu hiyo unaelekea ukingoni  na kufafanua kuwa viongozi hao watafanyiwa tathmini na kamati ndogo ya maadili ili kubaini kama walitekeleza ipasavyo adhabu hiyo.

 
Makada hao walipewa adhabu hiyo ya onyo kali na Kamati Kuu Februari 18, mwaka jana baada ya kuthibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea urais kabla ya wakati kinyume na kanuni za uongozi na maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).
Vilevile baada ya kuhojiwa, walithibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii.
Kutokana na adhabu ya onyo kali makada hao kwa mwaka mzima walikuwa katika hali ya kuchunguzwa ili kuwasaidia katika jitihada za kujirekebisha.
Pia kamati ndogo ya udhibiti iliagizwa kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine (mawakala na wapambe), kufanyika kwa vitendo hivyo vilivyovunja kanuni za chama.
Makada hao waliokuwa chini ya adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri wa Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Kwa nyakati tofauti jana, makada hao walizungumza na gazeti hili na kueleza kuwa wanasubiri kauli ya chama hicho baada ya adhabu yao kumalizika.
Kauli ya Nape
Akizungumza na gazeti hili jana Nape alisema, “Kanuni zetu zipo wazi. Adhabu ikimalizika itafanyika tathmini ili kubaini utekelezaji wa adhabu kwa wahusika.”
Hata hivyo, Nape alisema hakuna muda maalumu wa kufanya tathmini hiyo na kusisitiza kuwa inaweza kufanywa kwa siku moja, wiki au miezi, “Itategemea kazi yake itamaliza lini. Kamati ikimaliza kazi yake itawasilisha ripoti katika vikao vya juu vya chama.”
Nape alisisitiza kuwa adhabu kwa viongozi hao ilianza pale ambapo waliambiwa kuwa wamepewa adhabu, alipotakiwa kutaja tarehe ambayo walianza adhabu hiyo alisema kuwa haikumbuki, ila ilikuwa mwaka jana mwezi kama huu

No comments:

Post a Comment