Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, February 7, 2015

Mbasha Amkataa Mtoto Baada ya Flora kujifungua Asema ana mtoto Mmoja tu mwenye umri wa Miaka 10


Baada ya kusambaa kwa picha pamoja na habari kuwa mwanamuziki wa injili Flora Mbasha amejifungua na mwenyewe kulithibitisha hilo katika vyombo vya habari, mume wake Emmanuel Mbasha amemkana mtoto aliyezaliwa.
Akizungumza na kipindi cha Sunrise cha Times fm asubuhi ya jana, Mbasha amesema ana mtoto mmoja tu mwenye miaka 10 hiyo ikimaanisha hatambui uwepo wa mtoto aliyezaliwa hivi karibuni ambaye amezua minong'ono tena ikimuhusisha mchungaji Gwajima.
''Kwani wewe umesikia wapi habari hizo..mbona mimi sina! Kama ni kweli kajifungua basi mimi nampa hongera sana'' alisema Mbasha. 



Hata hivyo Mbasha akagoma kabisa kuendelea kuzungumzia suala hilo akisema litafika wakati wake ambao kila kitu kitakuwa wazi lakini watu waelewe ana mtoto mmoja tu.
Akizungumzia kuhusu ndoa yake na Flora,Mbasha amesema bado anatambua kuwa ndoa yao ipo licha ya kwamba mke wake anataka talaka.

Amemtaka Flora kurudi nyumbani na waendelee na maisha yao kama kawaida ikiwa ni njia ya kuharibu mipango ya shetani kama ilivyo jina la wimbo wake mpya alioutoa"Tunaharibu mipango ya shetani"

Flora kulia na mtoto wake

No comments:

Post a Comment