Mbeya. Katika kile kinachoonekana kutokuwa na imani na watu
waliojitokeza katika mchezo wa juzi kati ya Prisons na Yanga, baadhi ya
watu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa Mbeya City, waliingia lindoni baada
ya mchezo huo ili kulinda Uwanja wa Sokoine usiharibiwe.
Watu hao ambao walionekana kutokuwa na imani na
kila mtu aliyekuwa akikatiza katika nyasi za uwanja huo, walikuwa wakali
hata kwa shabiki maarufu wa Yanga anayetumia staili ya kujipaka masizi
usoni na kujaza nguo nyingi tumboni.
Gazeti hili lilishuhudia watu hao baada ya
mahojiano ya makocha wa Prisons na Yanga wakikataza watu kupitia hata
kando ya uwanja huo kwa kudai kuwa kuna imani za kishirikina.
Mmoja wa watu hao waliokuwa wakizuia watu bila
kutaja jina lake, aliliambia gazeti hili kuwa Yanga imefika Mbeya ikiwa
na watu wengi ,wakiwamo wazee wa klabu hiyo na hawatakubali kuchezewa
akili katika uwanja wao.
“Tupo hapa kwa ajili ya kuhakikisha uwanja
hauharibiwi kwa chochote, iwe imani za kishirikina au kwa njia nyingine,
wenzetu wamefungwa hapa na hatutaki na sisi kupoteza mchezo,” alisema
mtu huyo aliyekataa kutaja jina lake.
Aliongeza kuwa timu zao msimu huu ziko katika nafasi mbaya na wanahofia zote kupoteza michezo hiyo miwili dhidi ya Yanga
No comments:
Post a Comment