amemkosoa
Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), kwa kujiita ‘nyoka wa makengeza’ kwa
madai kwamba, anastahili kuitwa ‘nyoka wa ufisadi’.
Mnyika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema
wananchi wanapaswa kumuita Chenge ‘nyoka wa ufisadi’ badala ya kujisifia
kuwa ni ‘nyoka mwenye makengeza’ kwa kuwa amehusika katika kutafuna
mali ya umma.
“Kauli ya Chenge kama ilivyokuwa kwa ile ya ‘vijisenti’, ni kiburi cha kifisadi,” alisema Mnyika.
Chenge alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mahaha kata ya
Vunamala, wilayani Bariadi, mkoani Simiyu, akiwaeleza wananchi wa jimbo
lake kuwa aitwe nyoka kwa kuwa ni mjanja wa kutafuta fedha kwa ajili ya
wananchi wake.
Mnyika alisema udhaifu wa serikali na vyombo vyenye mamlaka ya
kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya tuhuma za ufisadi unaodaiwa
kufanywa na Chenge na watuhumiwa wengine wa ufisadi ndiyo unaowalinda
nyoka wa ufisadi na sasa wanajigamba kuwa ni wajanja wa kutafuta fedha
kifisadi.
“Chenge anadai kwamba yeye ni mjanja wa kutafuta fedha za wananchi
wa jimbo lake ili hali yeye na wenzake wamesababisha wananchi wa jimbo
lake na mengine nchini kukosa fedha nyingi zaidi za miradi ya maendeleo
mpaka hivi sasa kutokana na ufisadi wa Tegeta-Escrow,” alisema Mnyika.
Alisema Rais Jakaya Kikwete anapaswa kujitokeza tena kulihutubia
taifa kueleza hatua, ambazo ameendelea kuzichukua kukamilisha kutekeleza
maazimio ya Bunge.
Mnyika alisema taarifa alizonazo hadi sasa wapo washirika wa
maendeleo, ambao wameacha kutoa fedha kwa kutoridhika juu ya utekelezaji
wa maazimio ya Bunge kuhusiana na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.
Aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupamana na Rushwa (Takukuru) kuweka
wazi kwa umma matokeo ya uchunguzi wake na hatua zaidi zichukuliwe dhidi
ya wahusika
No comments:
Post a Comment