Serikali ya Jordan imewauwa wapiganaji wawili wa kiislamu,
waliokuwa wamezuiliwa korokoroni nchini humo na ambao Islamic State ilitaka
wabadilishane na rubani aliyechomwa moto pamoja na mwanahabari wa Japan ambaye
aliuwawa juma lililopita.
Msemaji wa Serikali Mohammad al-Momani, amesema kuwa
waliouwawa ni mlipuaji mmoja wa kike raia wa Iraqi Sajida al-Rishawi na mfuasi
wa Al-Qaeda, Ziad al-Karboli.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameungana na
mataifa mbalimbali duniani kulaani mauaji ya rubani huyo yaliyofanywa na
kikundi cha Islamic State, ambacho pia kinajulikana kama Daesh.
Rubani huyo alikamatwa ndege yake ilipoanguka katika
makabiliano na wapiganaji wa IS nchini Syria mwezi disemba.
Jordan ilijaribu kumuokoa luteni Kasasbeh katika ubadilishanaji
uliomuhusisha Rishawi.
Alikuwa amehukumiwa kunyongwa kufuatia msururu wa
mashambulizi katika mji mkuu wa Jordan Amman ambayo yaliwaua watu 60 mwaka
2005.
No comments:
Post a Comment