Mshambuliaji wa zamani wa FC Barcelona na timu ya Taifa ya
Uholanzi Patrick Kluivert alizungumzia ujio wa magwiji FC Barcelona nchini
mwezi wa tatu mbele ya waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Sports Lounge
uliopo jijini Dar Es Salaam ,Pembeni ya Kluivert ni mwenyekiti wa DRFA Ndugu
Almas Kasongo. Magwiji hao wa Barcelona wanataraji kucheza na wachezaji nyota
wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa mnamo mwezi wa machi tarehe 28.
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar Es Salaam,Almasi
Kasongo akizungumza kwenye
mkutano huo katikati na mwakilishi wa FC Barcelona
pamoja na Mwakilishi wa kampuni ya Prime Time Promotions Stuart Kambona ambao
ni waratibu wa mchezo huo
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo mapema leo
asubuhi
No comments:
Post a Comment