10. Elizabeth Michael ‘Lulu’
Binti huyu ana umri wa miaka 21 lakini ni mrembo na anayejiamini. Ni
binti kutoka Tanzania mwenye kipaji cha kuigiza kiasi cha kuwa tishio
kwa wakongwe. Ni kweli huwa anatumia ‘make up’ lakini hata akiwa
hajatumia wala kuvaa ‘mawig’, bado anaonekana ni mwenye kuvutia.
Tasnia ya filamu Afrika inakuwa kila siku kiasi kwamba zile ndoto za kufanya kama wenzetu wa Hollywood (Marekani) na Bollywood (India) huenda siku moja zikatimia.Kama ilivyo Hollywood na kwingine kwenye waigizaji wa kike wenye mvuto, wapo pia waigizaji wa kike Afrika ambao ni ‘visu’.Leo hii ikihitajika Top 10, kila mmoja atakuwa na yake lakini mtandao wa umefanya kazi ya kuorodhesha waigizaji 10 wa kike wenye mvuto kama ifuatavyo;
Tasnia ya filamu Afrika inakuwa kila siku kiasi kwamba zile ndoto za kufanya kama wenzetu wa Hollywood (Marekani) na Bollywood (India) huenda siku moja zikatimia.Kama ilivyo Hollywood na kwingine kwenye waigizaji wa kike wenye mvuto, wapo pia waigizaji wa kike Afrika ambao ni ‘visu’.Leo hii ikihitajika Top 10, kila mmoja atakuwa na yake lakini mtandao wa umefanya kazi ya kuorodhesha waigizaji 10 wa kike wenye mvuto kama ifuatavyo;
Ni mmoja wa mastaa wa kike nchini Nigeria mwenye mvuto wa aina yake. Kwa
sasa ana umri wa miaka 37 na watoto wanne lakini bado anaonekana mrembo
kiasi cha baadhi ya mashabiki wake kumuita Omosexy.Kutokana na kipaji
alicho nacho, amejikuta akiwa na mashabiki wengi katika Bara la Africa
na kwingineko duniani. Mbali na uigizaji pia ni mwanamitindo na
mwananamuziki.
Huyu ni muigizaji anayetokea nchini Ghana. Katika orodha ya waigizaji wa
kike waliomo nchini humo,
mrembo huyu amebaki kuwa tishio na imemfanya kuingia katika orodha hii ya wasanii wa kike wakali Afrika.
mrembo huyu amebaki kuwa tishio na imemfanya kuingia katika orodha hii ya wasanii wa kike wakali Afrika.
Huyu ni muigizaji kutoka Tanzania mwenye mvuto wa aina yake. Kwa mujibu
wa maelezo yake, uzuri alionao unatokana na mfumo mzuri wa kula
aliojiwekea. Anakula sana mbogamboga, matunda na maji mengi, hali
inayomfanya autunze urembo alionao.
6. Genevieve Nnaji
Ana umri wa miaka 36, anatokea Nigeria. Mwanadada huyu anatajwa kuwa na
mvuto wa aina yake kiasi cha kupata usumbufu kutoka kwa wanaume
kibao.Ameigiza filamu nyingi na zote amezitendea haki kutokana na namna
anavyouvaa uhusika.
5. Jackie Appiah Agyemang
Amezaliwa miaka 32 nchini Canada lakini amekulia nchini Ghana. Ni binti
mrembo na mwenye kipaji ambaye aonekanapo kwenye televisheni,
huthibitisha kwamba kuna kitu cha ziada alichojaaliwa na Mungu.
4. Nadia Buari
Huyu ni msanii kutoka Ghana aliyezaliwa miaka 30 iliyopita. Licha ya
umri kusogea, hachuji kwa uzuri. Amecheza filamu nyingi na kadiri siku
zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kuwa tishio kwenye tasnia ya uigizaji.
3. Ini Edo
Hivi unaanzaanzaje kumuacha mrembo huyu pale unapotaja medemu wakali
kwenye tasnia ya filamu Afrika? Naamini huwezi, labda uwe na chuki zako
binafsi.Ana umri wa miaka 31 na ana uzuri wa asili unaomfanya atumike
kwenye filamu nyingi za Nigeria.
2. Stephanie Okereke Linus
Huyu ni binti kutoka Nigeria ambaye wengi wanamtaja kuwa muigizaji
mwenye mvuto kuliko wote Afrika. Ana miaka 33, aliwahi kushiriki
mashindano ya urembo nchini Nigeria na kuibuka mshindi. Kuanzia hapo
amekuwa gumzo kwa uzuri wake na amekuwa akitumika sana kwenye filamu
nyingi.
1.Rita Dominic
Wafuatiliaji wa filamu za Nigeria watakuwa wanamjua vizuri binti huyu.
Ana miaka 40 lakini bado anadai. Kila sehemu ya mwili wake ina muonekana
wa kiurembo.
Angalia midomo yake, angalia macho na ngozi yake. Hakika ni kati ya waigizaji wa kike Afrika wenye mvuto wa aina yake.
No comments:
Post a Comment