Somo la ngono Uingereza
Shule zote za serikali zikiwemo za msingi na zile za upili
nchini Uingereza zitalazimika kufunza somo la ngono na uhusiano SRE ,wabunge wa
taifa hilo wamesema katika ripoti yao.
Kamati ya elimu katika bunge la Uingereza ilianzisha
uchunguzi baada ya kubainika kuwa zaidi ya thuluthi moja ya shule zilikuwa
zikishindwa kutoa mafunzo ya somo hilo kwa aumri unaohitajika.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Graham Sturat amesema
kuwa vijana
wadogo wana haki ya kupata habari ambazo zitahakikisha usalama wao.
Serikali imesema kuwa itaangazia matokeo ya ripoti hiyo.
Mwaka 2013 ripoti ya bunge hilo ilisema kuwa masomo ya
kibinafsi,ya kijamii ,afya na elimu ya kiuchumi ambapo somo hilo la ngono
limehusishwa yanahitaji kuimarika katika asilimia 40 ya shule.
Wabunge hao wamesema:Hali hii haitakubalika katika masomo
mengine licha ya kuwa harakati za serikali kuimarisha masomo hayo ni za kiwango
cha chini.
Je,unakubaliana na wazo la bunge la Uingereza kuwafunza
watoto wa shule za msingi somo la ngono na uhusiano? CHANZO bbcswahili.
No comments:
Post a Comment