Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 31, 2015

PICHA 10:::ASKOFU GWAJIMA AACHIWA KWA DHAMANA

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa kwenye baiskeli maalum ya wagonjwa Hospitali ya TMJ Dar es Salam leo mchana, wakati akielekea Kituo cha Polisi cha Oyterbay kupewa dhamana.
Hapa Askofu Gwajima akiingia kwenye gari huku akiwa na maumivu makali wakati akielekea kwenye kituo hicho kupewa dhamana
Wanahabari wakitoka kituo cha polisi Oysterbay kufuatilia 
habari hiyo.
Wachungaji wakibadilishana mawazo wakati wakimsubiri Askofu Gwajima apewe dhamana

 
Waumini wa kanisa hilo wakijiandaa kumpokea Askofu wao 
baada ya kupatiwa dhamana
waumini hao wakiwa kituoni hapo.
Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wakiwa wamelizonga gari lililombena Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Josephat Gwajima, huku wakishangilia kwa kusema yesu yesu baada ya kupewa dhamana  katika Kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo mchana.
Waumini hao wakilipungia mkono gari lililomchukua 
Askofu Gwajima. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment